Tuesday 9 April 2013

Maandalizi ya harusi(Wedding preparations)

Dear Groom and Bride
Mambo?
Kuna vitu vichache nimetamani kushirikiana na nyinyi leo kuhusiana na maandalizi ya Harusi.
1.Panga unavyotaka harusi yenu iwe na tarehe ya harusi ikiwezekana muambizane na Rangi

2.Kanisa na Ukumbi. Hivi vinaenda pamoja kwa kuanzia mwenye harusi mwezi wa Tisa naweza Kumrahisishia mawasiliano ya Kumbi za DAR-ES-SALAAM Wilaya Ya Kinondoni zote na chache za wilaya ya Ilala

3.Angalia kwa kifupi rough budget kama inawezekana  mjue mahitaji ya kumbi na Masharti yake,Uwezo wa kubeba watu na jiangalie wewe na uhusiano wako na watu kama unao wengi au wachache au wa kawaida

4.Anza kuangalia Mavazi na mkubaliane kuhusu mambo yatakayo pendezesha siku yenu,kwa kuangalia pia na uwezo....Vitu  hivyo ni:

  • Wasimamizi (Best man na Matron),mchague wenyewe kwa kukubaliana 
  • Bridesmaids na Grooms men..mjue rough cost ya kuanzia nguo saloon mpaka viatu
  • Rangi,uangalie uwezo wako na Rangi unazochagua ,matu wanaweza kuzipata je?watapendeza?
5.Tafuta keki na uwe na uhakika nayo,ikiwezekana kaonje kabla kama unaweza jua ladha

6.Muwe na uhakiwa wa saloon,na mkiweza kuangalia wenzenu wanafanya nini.

NB;Kipindi harusi yako inakaribia ndio muda wa kwenda kwenye harusi nyingi uwezavyo uige mazuri na ujifunze kutokana na makoda ya wenzako.



No comments:

Post a Comment